James Eduma.
Dar Es Salaam,Tanzania.
Uongozi wa klabu ya Simba umetoa shukurani
kwa mashabiki na wanachama wao kwa ustaarabu waliouonyesha wakati wa mchezo wao
dhidi ya Young Africans ambao ulimalizika kwa kupata ushindi wa mabao mawili
kwa moja.
Shukurani kwa mashabiki na wanachama wa
Simba zimetolewa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliono Haji Manara
alipozungumza na vyombo vya habari mchana wa leo kwenye ukumbi wa kamao makuu
ya klabu hiyo yaliopo Mtaa wa Msimbazi Dar es salaam.
Haji amesema mashabiki na wanachama wa
Simba walionyesha ustaarabu wa hali ya juu kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa
dhidi ya kikosi chao ambayo yalikua halali tangu dakika ya kwanza hadi mwisho.
Hata hivyo Haji Manara ametoa wito kwa
mashabiki na wanachama wa Simba kuendelea kuwa kitu kimoa katika kipindi hiki
cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu, na pia amewataka kufika viwanjani bila
kusita kuishangilia timu yao ili iweze kuhitimisha azma ya kutwaa ubingwa kwa
kushinda michezo saba ya ligi iliyobaki.
Wakati huo huo Manara ametoa shukurani kwa
Serikali, taasisi na watu mbali mbali ambao walihakikisha mchezo wa jumamosi
unachezwa kwa amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment