Bastia,Ufaransa.
MONACO imeshindwa kutanua wigo wake wa pointi na kufikia pointi sita kati yake na mabingwa watetezi, Paris Saint-Germain baada ya Ijuma usiku kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na wachovu Bastia huko Armand Cesari stadium, Bastia
Sadio Diallo alianza kuipa Bastia uongozi baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 19 ya mchezo kwa kichwa akiunganisha krosi ya Pierre Bengtsson.
Lakini alikuwa ni Mreno, Bernardo Silva aliyeipa Monaco ahueni ya kukwepa kichapo baada ya kufunga bao safi la kichwa katika dakika ya 52 akiunganisha krosi ya Almamy Toure.
Sare hiyo imeifanya Monaco ikae kileleni kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mabingwa watetezi, Paris Saint-Germain ambao Jumapili watashuka dimbani kucheza na Toulouse.
0 comments:
Post a Comment