Na Faridi Miraji.
-Serengeti boys itashiriki michuano ya Africa chini ya miaka kumi na Saba AFCON U17 Katika maandalizi ya kushiriki Waziri wa Habari, Sana'a utamaduni na Michezo Nape Nauye Leo ametangaza kamati ya watu kumi ya kusaidia maandalizi ya Serengeti boys.Waziri Nape amesema kazi kubwa ya kamati Hii ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu.
-Kamati hiyo Itakuwa chini ya Mwenyekiti Charles Hillary Mwanahabari mkongwe kutoka azam TV., Katibu wa kamati atakuwa Katibu wa shirikisho la Tanzania TFF Selestine Mwesigwa Huku wajumbe wakiwa wanamziki Alikiba na Diamond , wengine ni Maulid Kitenge, Ruge Mtabaha, Erick Shigongo , Hassan Abbas, Beatrice Singano na Mwanamitindo Hoyce Temu.
0 comments:
Post a Comment