Klabu ya soka ya Yanga imelitaka shirikisho la soka nchini kupitia kamati yake ya Sheria na hadhi ya wachezaji kuipitia upya hukumu iliyotolewa kuhusu beki wao wa kulia Hassani Ramadhani Kessy.
Hukumu iliyotolewa mwezi Desemba na kamati hiyo , inawataka Yanga SC kuilipa klabu ya Simba SC fidia ya shilingi milioni 50 kwa kumsainisha mchezaji huyo ilihali akiwa bado hajamalizia mkataba wake na wekundu hao wa Msimbazi. Sambamba na hilo Yanga inatakiwa kutoa faini ya shilingi milioni 3 kwa shirikisho la soka nchini.
Kupitia mwanasheria wake , Yanga imewataka TFF kupitia upya hukumu hiyo katika kikao kinachokaa jumapili
0 comments:
Post a Comment