Brussels, Ubelgiji.
KRC Genk ya Mtanzania,Mbwana Samatta,jana Jumamosi iliionja joto ya jiwe ugenini baada ya kuchapwa virungu viwili vya nguvu bila majibu (2-0) na wenyeji wao RSC Anderlecht kwenye mchezo mkali wa ligi kuu Ubelgiji uliochezwa huko kwenye dimba la Constant Vanden Stock mjini Brussels,Ubelgiji.
Mabao ya RSC Anderlecht yamefungwa na beki Msenegali, Serigne Modou Kara Mbodji dakika ya 3 na kiungo Mbelgiji, Yoeri Tielemans dakika ya 50.
Ushindi huo umeifanya RSC Anderlecht ifikishe pointi 58 ikiwa imecheza mechi 28 na inaendelea kukaa nafasi ya pili, nyuma ya vinara Club Brugge yenye pointi 58 lakini wana uwiano mzuri wa mabao.
KRC Genk imeshuka mpaka nafasi ya nane ikiwa na pointi zake 42 baada ya michezo 28.
0 comments:
Post a Comment