728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 17, 2017

    Tanzia:Kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars ya Maximo afariki dunia

     

    Mbeya,Tanzania.

    KIUNGO wa zamani wa Yanga na Taifa Stars,Geoffrey Bony Mandanje,amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rungwe mkoani Mbeya alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

    Dada wa marehemu Neema Boniface, amesema kuwa Bony alianza kuumwa
    ugonjwa usiojulikana miezi mitatu iliyopita na mpaka anafariki bado haikujulikana alikuwa akiumwa ugonjwa gani.
     

    Bony aliyeimudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji alijiunga na Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000 akitokea Tanzania Prisons na kuwa tegemeo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa chini ya Mbrazil Marcio Maximo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Tanzia:Kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars ya Maximo afariki dunia Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top