Munich,Ujerumani.
BAYERN Munich imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ya Bundesliga baada ya jioni hii kuichapa Hamburg SV kwa jumla ya mabao 8-0 nyumbani Allianz Arena.
Shujaa katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Poland,Robert Lewandowski, aliyefunga mabao matatu [ hat trick] na kufikisha hat trick tatu msimu huu huku jumla akiwa amepachika mabao 19.
Mabao mengine ya Bayern Munich katika mchezo wa leo yamefungwa na Arturo Vidal ,David Alaba, Kingsley Coman aliyefunga mabao mawili pamoja na Mdachi Arjen Robben.
Ushindi huo mnono umeifanya Bayern Munich ikae kileleni kwa pointi tano zaidi mbele ya RB Leipzig inayoshika nafasi ya pili.
Matokeo mengine:RB Leipzig imeifunga Cologne mabao 3-1 kwa mabao ya Werner,Emil Forsberg na Dominic Maroh.Bao la Cologne limefungwa na Yuya Osako.
Borussia Dortmund imeichapa Freiburg mabao 3-0.Shukrani kwa mabao ya Sokratis Papastathopoulos na Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga mabao mawili na kufikisha mabao 19 sawa na Robert Lewandowski.
Bayer Leverkusen imenyukwa mabao 2-0 na Mainz kwa mabao ya Stefan Bell na Levin Oztunali.
Augsburg imetoka nyuma na kuichapa Darmstadt, mabao 2-1 kwa mabao ya Paul Verhaegh na Raul Bobadilla.Bao la Darmstadt limefungwa na Marcel Heller.
0 comments:
Post a Comment