Na Faridi Miraji.
Manchester,England.
Joe Hart ataruhusiwa kujiunga na klabu mojawapo kati ya zile zilizo nafasi sita za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza msimu ujao kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Telegraph.
Baada ya kutua Manchester City mapema majira ya kiangazi yaliyopita Pep Guardiola aliamua kumbadili Hart kwa Claudio Bravo , lakini kocha huyo anajiandaa kumruhusu Hart kuondoka kwa ada isiyopungua pauni milioni 20.
Arsenal na Liverpool wamekuwa wakihusishwa na Kipa huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye msimu huu anacheza kwa mkopo katika klabu ya Torino nchini Italia.
0 comments:
Post a Comment