Na Faridi Miraji
Kocha wa Monaco Leonardo Jardim amekiri kwamba siku moja anatamani kufundisha klabu katika ligi kuu ya Uingereza hasa baada ya kuhusishwa na kuhamia Arsenal.
Jardim ameripotiwa kuwa kwenye orodha inayounda makocha wanne wanatajwa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger ambao ni Thomas Tuchel, Roger Schmidt na Massimo Allegri, kama Mfaransa huyo ataondoka Emirates mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa sasa wa Wenger unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu na bado hakuna makubaliano kama ataendelea na utawala wake wa miaka 20 katika jiji la London.
Akiongea kuelekea kwenye mechi ya UEFA hatua ya 16 bora dhidi ya Manchester City, Jardim alisema," Makocha wote na wachezaji wote Duniani wanapenda kufanya kazi katika ligi na vilabu vya kiwango cha Dunia."
"Ligi kuu ya Uingereza ni ligi muhimu sana, tena labda ni muhimu kuliko zote Ulaya. Kila mtu siku moja angependa kupata fursa ya kufanya kazi Uingereza."
"Lakini pia tuna mradi wetu hapa Monaco. Tuna jukumu katika hii klabu. Kwangu mimi kwasababu ya heshima ya hii klabu , najitolea kwa asilimia 200 ili kupata mafanikio."
0 comments:
Post a Comment