Leceister,England.
IKICHEZO mchezo wake wa kwanza bila ya kocha wa Claudio Ranieri aliyetimuliwa wiki iliyopita,Leceister City imepata ushindi wake wa kwanza tangu kuanza kwa mwaka 2017 baada ya Jumatatu usiku kuifumua Liverpool kwa mabao 3-1 katika mchezo pekee wa ligi kuu England uliochezwa huko King Power Stadium.
Jamie Vardy ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za 28 na 60 huku kiungo Danny Drinkwater akifunga bao moja katika dakika ya 39.Bao la Liverpool limefungwa na Philippe Coutinho katika dakika ya 68.
Ushindi huo umeifanya Leceister City ifikishe pointi 24 na kuchupa mpaka nafasi ya 15.Liverpool imebaki katika nafasi ya 5 na pointi zake 49.Timu zote zimecheza michezo 26 kila moja.
0 comments:
Post a Comment