Sevilla,Hispania.
SEVILLA wametoka nyuma na kuwachapa watani wao wa jadi Real Betis mabao 2-1 kwenye mchezo mkali wa La Liga wa 'El Gran Derbi' uliochezwa kwenye dimba la Estadio Benito Villamarin ,Jumamosi usiku.
Wenyeji Real Betis ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya mlinzi wake wa kushoto, Riza Durmisi kufungwa kwa mkwaju wa faulo katika dakika ya 36 ya mchezo.
Lakini mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha wa Sevilla, George Sampaoli ya kuwaingiza nahodha Vicente Iborra na Wissam Ben Yedder yaliipa matumaini miamba hiyo ambapo ilifanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Gabriel Mercado katika dakika ya 56 na Vicente Iborra kwa kichwa katika dakika ya 76 ya mchezo.
Ushindi huo umeifanya Sevilla ichupe mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya La Liga ikiwa na pointi 52 sawa na vinara Real Madrid wenye michezo miwili mikononi.Mabingwa watetezi Barcelona wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 51.
Michezo ya leo La Liga
Atletico Madrid v Barcelona 12:00 jioni
Virrareal v Real Madrid
0 comments:
Post a Comment