728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 17, 2017

    Liverpool kuchomoa mmoja Chelsea kwa Pauni Milioni 8

    Liverpool, England.

    LIVERPOOL imepanga kuishtua Chelsea katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya kwa kumsajili mshambuliaji wake kinda aliyegomea mkataba mpya klabuni hapo,Dominic Solanke.

    Hivi karibuni Solanke mwenye umri wa miaka 19 aliripotiwa kugomea mkataba mpya wa kuendelea kusalia Stamford Blidge baada ya Chelsea kukataa kumpa ofa ya mshahara wa Pauni 50,000 kwa wiki.

    Gazeti la The Sun limesema kocha wa Liverpool,Jurgen Klopp ni shabiki mkubwa wa soka la Solanke na yuko tayari kumsajili ili kuchukua nafasi ya Daniel Sturridge atakayeuzwa mwishoni mwa msimu huu.

    Tayari Solanke ameshawaambia marafiki zake wa karibu kuwa katika dirisha lijalo la usajili ataihama Chelsea na kutua Liverpool ili akapate nafasi ya kuendeleza kipaji chake.

    Hata hivyo licha ya mkataba wa Solanke kuwa ukingoni,Liverpool italazimika kuilipa Chelsea kitita cha Pauni Milioni 8 kama fidia kwa kuwa kinda huyo ana umri wa chini ya miaka 24.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Liverpool kuchomoa mmoja Chelsea kwa Pauni Milioni 8 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top