Southampton,England.
MCHEZO wa ligi kuu England uliokuwa uchezwe mwanzoni mwa mwezi Machi kati ya Manchester United na Southampton umeahirishwa.
Sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili ya Machi 12 huko Saint Mary's zimedaiwa kuwa ni kuingiliana kwa ratiba ya michezo ya ligi kuu na ile ya kombe la FA ambapo timu zote mbili zimefuzu hatua ya robo fainali.
Ikumbukwe michezo ya kombe la FA imepangwa kuchezwa kati ya Machi 10 na 13 mwaka huu hivyo kufanya baadhi ya michezo ya ligi kuu kuahirishwa.
Wakati huohuo Southampton pia bado wanasubiri tarehe mpya ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Arsenal ambao pia uliashirishwa wikendi iliyopita kutokana na kuingiliana na ratiba ya kombe la FA
0 comments:
Post a Comment