AZAM FC imewapa zawadi nzuri ya wikendi mashabiki wake baada ya usiku huu kuichapa Mwadui FC kutoka Shinyanga mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu bara ulioisha hivi punde huko Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.
Mpaka mapumziko Azam FC ilikuwa mbele kwa bao moja lililotiwa kimiani katika dakika ya 24 na kiungo fundi Salum Abubakar 'Sure Boy' kwa mkwaju mkali wa mbali baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Frank Domayo.
Kipindi cha pili walikuwa ni Azam FC tena walioendelea kucheka baada ya kuongeza bao la pili katika dakika ya 88 kufuatia mlinzi wa kati wa Mwadui FC,Iddy Mobby kujifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira uliotemwa na kipa wake,Shaaban Kado, aliyekuwa akiokoa krosi iliyochongwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ na kufanya matokeo yawe 2-0 mpaka mwisho.
Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe pointi 41 baada ya kushuka dimbani mara 23 na kuendelea kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikizidiwa pointi 10 na kinara Simba yenye pointi 51 ambayo ina mchezo mmoja mkononi.
Vikosi
Azam FC:Aishi Manula,Shomary Kapombe, Bruce
Kangwa, Abbrey Morris,
Yakubu Mohammed, Himid
Mao, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’/Samuel Afful dk62,
Frank Domayo, Yahya
Mohammed/Erato Nyoni
dk88, Ramadhani Singano
‘Messi’ na Joseph
Mahundi/Masoud Abdallah
‘Cabaye’ dk70.
Mwadui FC; Shaaban Kado,
Nassor Masoud ‘Chollo’,
David Luhende, Iddi Mobby,
Malika Ndeule, Razack
Khalfan, Abdallah Seseme,
Awadh Juma, Paul Nonga/
Salum Iyee dk18, Miraj
Athuman na Hassan Kabunda.
0 comments:
Post a Comment