728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 17, 2017

    Mashabiki Chile wapanga kuandamana kumwomba Alexis Sanchez ahame Arsenal.

    Santiago,Chile.

    MAELFU ya mashabiki wa soka nchini Chile wamepanga kufanya maandamano nchi nzima ili kumwomba Alexis Sanchez kuihama Arsenal kwa kile kinachodaiwa kuwa staa wao hapewi sapoti ya kutosha klabuni hapo.

    Mashabiki hao wameripotiwa kutumia mtandao wa Facebook kuyapa nguvu maandamano hayo ambayo yamepangwa  kufanyika kwenye mji wa mkuu wa Chile,Santiago siku ya Machi 1.

    Maandamano hayo yatakayofahamika kama "Maandamano ya kitaifa ya kumwomba Alexis
    Sanchez ahame Arsenal'' -tayari yameshapata baraka za mashabiki 4,000 mpaka sasa.

    Akinukuliwa mmoja wa mashabiki waandamizi wa maandamano hayo amesema wao kama mashabiki wa Chile wamechoka kumwona staa wao akipambana peke yake kuhakikisha anaipa Arsenal matokeo mazuri wakati wengine wakiwa wanamtazama tu.

    (Hatutaki aende Real Madrid au arejee Barcelona,hatutajali anakwenda wapi tunachotaka ni kuona Sanchez pamoja na wachezaji wengine kumi wanapambana kuipa timu matokeo mazuri.Hastahili kuwa peke yake)
    .

    Hatua hiyo imefikiwa muda mfupi baada ya Arsenal kulambwa mabao 5-1 na Bayern Munich kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mashabiki Chile wapanga kuandamana kumwomba Alexis Sanchez ahame Arsenal. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top