728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 28, 2017

    Waamuzi Yanga,Zanaco wawekwa hadharani.

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SHIRIKISHO la vyama vya soka barani Afrika (CAF) leo limetaja majina ya waamuzi wanne watakaochezesha mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania Yanga na mabingwa wa Zambia, Zanaco FC.

    Katika mchezo huo utakaochezwa Machi 11,2017 kwenye Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam,Mwamuzi Djamal Aden Abdi,47, kutoka Djibouti ndiye aliyepewa jukumu la kusimama kati akisaidiwa na Hassan Egueh Yacin na Farhan Bogoreh Salime ambao nao wanatokea Djibouti.

    Mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Ahmed Djamal kutoka Djibouti pia huku kamisaa wa mchezo akiwa Luleseged Begashaw Asfaw kutoka Ethiopia.

    Yanga na Zanaco zitarudiana tena wiki moja baadae huko Lusaka,Zambia na timu itakayokuwa imepata ushindi mkubwa zaidi ya nyingine itafuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Waamuzi Yanga,Zanaco wawekwa hadharani. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top