Na Faridi Miraji
Beki wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique amesema kwamba wachezaji wote wa klabu hiyo wapo nyuma ya kocha wao aliye kwenye presha kubwa, Luis Enrique.
Kichapo cha 4-0 kutoka kwa PSG kimeibua wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa Enrique katika dimba la Camp Nou, huku taarifa mbalimbali zikiarifu kwamba mabingwa hao wa La Liga wanafikiria kutafuta mbadala wa kocha huyo mwishoni mwa msimu huu.
Pique amemtetea kocha wake ambaye aliwaongoza kutwaa makombe matatu msimu wa 2014/2015 kwa kusema wachezaji wote wapo nyuma ya kocha wao.
"Na Luis Enrique tulikuwa kwenye nyakati mbaya na akatuongoza kutwaa mataji matatu."
"Najua mpira wa miguu hauna kumbukumbu, lakini ningependa tukumbuke nyuma na kuangalia kazi yote nzuri aliyoifanya hapo nyuma katika klabu hii. Nashindwa kuelewa kwanini watu wana kumbukumbu fupi sana. Na zaidi ya hapo kuna mafanikio mazuri aliwahi kuyapata akiwa mchezaji pia."
"Tupo na kocha wetu mpaka kifo. Kwa pamoja tutajaribu kusonga mbele."
0 comments:
Post a Comment