-Mchezaji bora wa ligi ya Vodacom (VPL) mwezi wa kumi na mbili Method Mwajale hatihati kuwavaa YANGA kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Tz Prison. Mwajale alipewa mapumziko ya siku kumi kuanzia tar 11/02/2017 mpaka Jumatatu ya tar 20/02/2017 alipojiunga na wenzake Zanzibar na kupewa program maalumu ambayo aliianza jumatatu . Ambapo Leo ataanza mazoezi Magumu na wenzake Kwa uangalizi maalumu ili kuaangalia uwezekano Kama atakuwa fiti mpaka jumamosi Huku kocha msaidizi wa SIMBA Jackson Mayanja akasema SIMBA inawachezaji wengi wazuri yoyote atakayepangwa atacheza vizuri.
VIONGOZI
-Viongozi wa SIMBA ambao walifika Jana kwenye kambi hiyo walikata tamaa juu ya utimamu wa Mwajale na kuanza kufanya mchakato wa kumsafirisha Juuko Murishid ili aungane na wenzake Kwa maandalizi ya mechi dhidi ya YANGA. Habar kutoka ndani ya uongozi walikuwa Tayar kumtumia denge binafsi ili aweze kuungana na wenzake sema tu mpango huo ulipingwa na kocha mkuu pamoja na meneja wa simba ambapo waliwaambia viongozi tuwaamini wachezaji waliopo tu Kwani Kwa sasa wana morali nzuri kuelekea mechi ya jumamosi tukimleta Juuko anaweza akashusha morali ya wachezaji waliopo.
-Kuna uwezekano Mkubwa beki ya Simba jumamosi kuanza Lufunga na Banda Huku Mwajale akianzia bechi. Ila viongozi wa simba hawana imani Sana na Novart Lufunga. Kikosi cha SIMBA kinaweza kuwa hivi
1-Agyei, 2-Bukungu, 3-Tshabalala, 4-Banda, 5-Lufunga, 6-Mkude, 7-Mzamiru, 8-Kotei, 9-Mavugo, 10-Ajibu, 11-Ndemla.
0 comments:
Post a Comment