Pretoria,Afrika Kusini.
MABINGWA wa Afrika ,Mamelodi Sundowns wameendeleza wimbi lao la kujinyakulia vikombe vikubwa Afrika baada ya leo jioni kuibanjua TP Mazembe ya DR Congo kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa kuwania ubingwa wa CAF Super Cup Afrika.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Loftus Versfeld huko Pretoria,Afrika Kusini ilishuhudiwa wenyeji Mamelodi Sundowns wakijipatia bao lao la pekee na la ushindi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 83 ya mchezo kupitia kwa mlinzi wake nyota Ricardo
Nascimento.
Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya mlinzi wa kushoto wa TP Mazembe,Issama Mpeko kumwangusha nahodha wa Mamelodi Sundowns,Hlompho Kekana ndani ya boksi na mwamuzi Ghead Grisha kutoka Misri kuamuru ipigwe penati ambayo ilifungwa kiufundi na Ricardo Nascimento.
Ubingwa huo ni wa pili kwa Mamelodi Sundowns msimu huu baada ya ule wa klabu bingwa Afrika iliyoutwaa kwa kuichapa Zamalek ya Misri kwenye fainali.
Vikosi
Mamelodi Sundowns: Denis Onyango,Thapelo Morena,Wayne Arendse,Ricardo Nascimento,Tebogo Langerman,Tiyani Mabunda,Hlompho Kekana,Themba Zwane,Anthony Laffor,Khama Billiat,Percy Tau
TP Mazembe:Sylvain Gbohouo,Djos Issama,Joel Kimwaki,Salif Coulibaly,Jean Kasusula,
Nathan Sinkala,Daniel Adjei,Rainford Kalaba,Solomon Asante,Ben Malango,Meschak Elia
0 comments:
Post a Comment