Manchester, England.
KOCHA Mreno,Jose Mourinho,ameungana na makocha Sir Alex Ferguson na Brian Clough katika orodha ya makocha waliotwaa ubingwa wa kombe la ligi mara nyingi zaidi [mara nne] baada ya jana Jumapili kuiongoza Manchester United kuilaza Southampton kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali wa kombe la ligi (EFL CUP) uliochezwa kwenye dimba la Wembley jijini London.
Kabla ya jana tayari Mourinho alikuwa ameshatwaa ubingwa huo mara tatu akiwa na Chelsea mwaka 2005, 2007 na 2015.
Ubingwa huo pia umemfanya Mourinho kuwa kocha wa kwanza wa Manchester United kutwaa kikombe akiwa katika msimu wake wa kwanza.
Mabao ya Manchester United kwenye mchezo wa jana yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic aliyefunga mabao mawili na Jesse Lingard aliyefunga bao moja.Mabao yote ya Southampton yalifungwa na Manolo Gabbiadini.
0 comments:
Post a Comment