Manchester, England.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City,Sergio Aguero,amewaambia watu wake wa karibu kuwa anataka kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.
Staa huyo wa Argentina yupo katika wakati mgumu baada ya kocha,Pep Guardiola,kuamua kumsugulisha benchi kwenye michezo minne mfululizo tangu kuwasili kwa kinda matata wa Brazil,Gabriel Jesus,19 akitokea Palmeiras.
Hivi karibuni Aguero,28,alidaiwa kufanya mazungumzo binafsi na kocha Pep Guardiola lakini akashindwa kuhakikishiwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City hali ilinayomlazimu kufikiria kuondoka klabuni hapo na kutua Real Madrid.
Hata hivyo Real Madrid italazimika kuvunja benki kwa ajili ya kumsajili Aguero kwani Manchester City imeripotiwa kuwa haitamwachia staa huyo kwa ada ya chini ya Pauni Milioni 60.
Aguero alijiunga na Manchester City mwaka 2013 akitokea Atletico Madrid ya Hispania kwa ada ya Pauni Milioni 35.
0 comments:
Post a Comment