Paul Manjale
Dar Es Salaam,Tanzania.
Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea tena keshokutwa
Jumatano ambako mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans itaalikwa
na Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mbali
ya mchezo huo mmoja kwa siku ya Jumatano, ligi hiyo ambayo ni michuano
mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya
Jumamosi Machi 4, mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Ukiacha
mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni
kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini
Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba.
Azam
FC pia itacheza Jumamosi Machi 4, mwaka huu na Stand United ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni
wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejesha tena mechi za Ligi Kuu
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa
Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa
mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo
mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako
African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
0 comments:
Post a Comment