London,England.
DROO ya robo fainali ya michuano ya Emirates FA CUP imepangwa usiku huu huko London,England baada ya sehemu kubwa ya michezo hiyo ya hatua ya 5 kukamilika.
Katika droo hiyo vinara wa sasa wa ligi kuu England,Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Blidge kuwaalika mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester United.
Tottenham watacheza na Millwall huku Middlesbrough wakitarajiwa kucheza na mshindi kati ya Huddersfield na Manchester City.Mshindi kati ya Sutton na Arsenal atacheza na Lincoln.
Michezo ya robo itachezwa kati ya Machi 11-13, 2017.
Ratiba Kamili
Chelsea v Manchester United
Middlesbrough v Huddersfield/Manchester
City
Tottenham v Millwall
Sutton/Arsenal v Lincoln
0 comments:
Post a Comment