Na Faridi Miraji.
Liverpool wanajiandaa kula sahani moja na Real Madrid kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa kimataifa wa Ujerumani Julian Brandt.
Klabu hiyo ya jiji la Merseyside wameripotiwa kutuma Maskauti kwenda kumuangalia Brandt,20 akiwa na kikosi chake cha Bayer Leverkusen kwenye mechi ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid jana usiku
Maendeleo ya ukuaji wa kasi wa kiwango cha soka cha Brandt yamevutia vilabu vingi vikubwa barani Ulaya ikiwemo Real Madrid, lakini Klopp ana matumaini ya kumpeleka winga huyo Anfield.
0 comments:
Post a Comment