Madrid,Hispania.
WATUMIAJI wa Facebook sasa wataweza kutazamaza live mechi za La Liga kupitia simu na kompyuta zao bila malipo yoyote yale.
Mpango huo umefikiwa na chama cha soka cha Hispania ili kutoa fursa kwa wapenzi wa ligi ya La Liga kuendelea kupata uhondo hata wanapokuwa mbali na televisheni zao.
Mchezo wa kwanza kuonyeshwa kupitia Facebook utakuwa ule wa leo Jumamosi mchana kati ya Granada na Real Betis na utaonyeshwa kupitia ukurasa rasmi wa La Liga pamoja na kituo cha televisheni cha Gol.
Taarifa iliyochapishwa kutoka mtandao wa La Liga imesema hatua hiyo ni matunda ya maendeleo yaliyoletwa na mfumo mpya wa urushaji matangazo wa kidigitali.
0 comments:
Post a Comment