Barcelona, Hispania.
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid,Mfaransa Kevin Gameiro ameingiza jina lake kwenye vitabu vya historia ya ligi ya La Liga baada ya jioni ya leo kufunga hat-trick ya mapema zaidi kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Sporting Gijon huko El Molinon.
Gameiro aliyekuwa ameingia uwanjani akitokea benchi alikamilisha hat-trick hiyo akitumia dakika nne na sekunde 51 na kuwa mchezaji wa pili kufunga hat-trick ya mapema zaidi kwenye historia ya ligi ya La Liga.Hat-trick hiyo imepatikana kwenye dakika za 80,81 na 85.
Rekodi ya hat-trick ya mapema zaidi inashikiliwa na nyota wa zamani wa Valencia,David Villa ambapo mwaka 2006 kwenye mchezo dhidi ya Atletic Bilbao alifunga hat-trick akitumia dakika nne na sekunde 41.
0 comments:
Post a Comment