728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 20, 2017

    Serikali yasema Waamuzi walivunja viti Taifa

    Na Faridi Miraji.                                              
    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SERIKALI imeitaka bodi ya ligi kupanga waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri sheria 17 za soka kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa ili kuzuia athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo uharibifu wa mali za uwanja.

    Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa michezo kutoka Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Yusuph Singo alipokuwa alizungumza na waandishi wa Habari kwenye mkutano maalum wa maandalizi ya mchezo huo kuwa kama hakutakuwa na waamuzi wazuri mechi inaweza ikatawaliwa na vurugu.

    Singo alisema kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba mosi mwaka jana na kushuhudiwa vurugu kubwa zilizopelekea viti 1781 kuvunjwa, zilitokana na maamuzi mabovu ya waamuzi wa mchezo huo.

    “Tunaitaka bodi ya ligi kupanga waamuzi wazuri kwenye mchezo huu kwakuwa unavuta hisia za watu wengi na pia tunawaomba mashabiki kuwahi mapema na kutojihusisha na vurugu zozote kwani ulinzi utakuwa wa kutosha” alisema Singo.

    Kwa upande mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Inspekta Hashim Abdallah alisema ulinzi utaimarishwa vya kutosha na wale wote watakaovunja sheria watachukuliwa hatua stahiki ukizingatia uwanja wa huo umefungwa kamera maalum kwa ajili ya ulinzi.

    “Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia timu zao kwa amani lakini watakao jihusisha na vurugu tutawashughulikia ipasavyo” alisema Inspekta Hashimu .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serikali yasema Waamuzi walivunja viti Taifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top