728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 22, 2017

    Man City yaizima Monaco 5-3 ligi ya mabingwa Ulaya

    Manchester,England.

    Manchester City imelazimika kutoka nyuma mara mbili na kufanikiwa kuichapa Monaco mabao 5-3 kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16boraa ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.

    Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Etihad,jijini Manchester, Raheem Sterling aliipa uongoza Manchester City baada ya kufunga bao la kuongoza dakika ya 26 akimalizia pasi nzuri ya Leroy Sane.



    Bo hilo liliwaamsha Monaco ambao walikuja juu na kuanza kuonyesha kandanda safi ambalo liliwapatia mabao mawili ya haraka yaliyofungwa na Radamel Falcao kwa kichwa dakika ya 32 na Kylian Mbappe kwa shuti kali dakika ya 40 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao hayo mawili.

    Kipindi cha pili kilianza kwa Falcao kukosa mkwaju wa penati uliochezwa na kipa wa Manchester City,Willy Caballero.Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la pili dakika ya 58 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 71.

    Mabao mengine ya Manchester City yamefungwa na mlinzi John Stones dakika ya 77 huku bao la nne likifungwa na mchezaji bora wa mechi Leroy Sane dakika ya 82.


    Timu hizo zitarudiana tena mwezi Machi huko Monaco na mshindi atafuzu hatua ya robo fainali.Katika mchezo mwingine Atletico Madrid ikiwa ugenini Bay Arena imewachapa wenyeji wao Bayer Leverkusen mabao 4-2.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Man City yaizima Monaco 5-3 ligi ya mabingwa Ulaya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top