Dar Es Salaam,Tanzania.
MABINGWA wa soka nchini na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya vilabu bingwa Afrika,Yanga SC leo jioni watawakosa nyota wao watatu pale watakaposhuka kwenye Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam kucheza na Ngaya Club de Mbe ya Comoro kwenye mchezo wao wa mkondo wa pili wa hatua ya mtoano.
Kocha msaidizi wa Yanga SC,Juma Mwambusi amewataja wachezaji hao kuwa ni Mzimbabwe Donald Ndoma,Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Mrundi Amissi Tambwe.
Mwambusi amesema wachezaji wote watatu ni wagonjwa,Ngoma bado anauguza jeraha la goti alilolipata kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi lililofanyika mwezi uliopita visiwani Zanzibar.
Niyonzima na Amissi Tambwe wao watakosekana kutokana na kupata majeruhi katika mchezo wa awali uliochezwa Jumamosi iliyopita huko Moroni,Comoro.
0 comments:
Post a Comment