728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 28, 2017

    Freddie Ljungberg aikacha Arsenal na kutua Ujerumani

    London, England.

    STAA wa zamani wa Sweden,Freddie Ljungberg amekikacha kibarua chake cha kukinoa kikosi cha vijana cha Arsenal cha U-15 na kutua Wolfsburg kwenda kuwa mmoja kati ya wasaidizi wa Andries Jonker ambaye ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo ya Ujerumani inayosuasua kwenye ligi ya Bundesliga.

    Ljungberg,39,alirejea Arsenal msimu uliopita baada ya kustaafu mwaka 2014 na kupewa jukumu la kuwa kocha wa kikosi cha vijana cha U15 kibarua ambacho alikifanya vizuri na kumvutia Jonker aliyekuwa akihudumu kama mkuu wa akademi ya Arsenal.



    Ljungberg alijiunga na Arsenal mwaka 1998 akitokea Halmstads BK.Aliichezea Arsenal kwa miaka minane akifunga mabao 71 katika michezo 313.Pia aliisaidia klabu hiyo ya kaskazini mwa London kushinda vikombe viwili ya FA na vikombe viwili vya ligi kuu England.Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichomaliza msimu wa 2003/04 bila kufungwa.

    Jonker ametua Wolfsburg kuchukua nafasi ya Valérien Ismaël aliyetimuliwa kibarua chake Ijumaa iliyopita baada ya Wolfsburg kuchapwa mabao 2-1 na Werder Bremen na kuukaribia zaidi mstari wa kushuka daraja.

    Jonker alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akiwa kama mkuu wa akademi kuchukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Liam Brady aliyejiuzulu.Kabla hapo Jonker aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Wolfsburg.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Freddie Ljungberg aikacha Arsenal na kutua Ujerumani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top