Madrid,Hispania.
LIONEL Messi ameibuka shujaa baada ya kuifungia Barcelona bao la pili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo mkali wa La Liga ulioisha hivi punde huko Vicente Cardelon.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi,Antonio Mateu,na kushuhudiwa na matazamaji 52,525 ilishuhudiwa mpaka mapumziko yakiwa sare ya bila kufungana licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili kilianza kuwa chema kwa Barcelona baada ya Rafinha Alcantara kuifungia bao la kuongoza katika dakika ya 64 baada ya kuuwahi mpira uliobabatizwa na mabeki wa Atletico Madrid na kufunga bao.
Katika dakika ya Atletico Madrid walipata bao la kusawazisha baada ya Diego Godin kufungwa kwa kichwa katika dakika ya 70 akiunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Koke.
Katika dakika ya 86 Lionel Messi aliihakikishia Barcelona ushindi baada ya kuifungia bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa karibu akimalizia kazi nzuri ya Luis Suarez aliyewahandaa walinzi wa Atletico Madrid.
Ushindi huo umeipeleka Barcelona kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kufikisha pointi 54.Pointi mbili mbele ya Real Madrid yenye pointi 52 na michezo miwili mkononi.
Vikosi
Atletico Madrid: Oblak; Vrsaljko, Godin, Savic,Filipe; Gabi, Koke, Saul, Carrasco (Torres 68);Griezmann, Gameiro (Correa 72)
Barcelona : Ter Stegen; Pique, Umtiti, Mathieu (Digne 77); Sergi (Gomes 85), Busquets,Iniesta (Rakitic 71), Rafinha; Messi, Suarez,Neymar
0 comments:
Post a Comment