728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 25, 2017

    Kiungo wa Malaga kumrithi Cazorla Arsenal (+Video)

    London, England.

    ARSENAL ni kama imeanza kukatishwa tamaa hivi na afya ya kiungo wake majeruhi,Santi Cazorla hii ni baada ya kuripotiwa kuanza kumfukuzia kiungo mahiri wa Malaga,Pablo Fornals Malla.

    Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania,habari zinasema Fornals,21, amejikuta akiingia kwenye rada za Arsenal baada ya Cazorla,32,ambaye pia alitokea Malaga kuendelea kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamefanya ashindwe kutumikia ipasavyo katika misimu miwili ya hivi karibuni.

    Habari zaidi zinasema tayari Arsenal imeshaanza mipango ya kutaka kumsajili Fornals katika majira yajayo ya joto.Ikiwa dili hilo litakamilika Fornals atakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Arsenal akitokea Malaga baada ya Cazorla.




    Msimu huu Fornals ameifungia Malaga mabao 4 na kupika mengine 2 katika michezo 18.Amekosa michezo mitano na katika michezo hiyo Malaga wameambulia ushindi katika mchezo mmoja pekee.

    Fornals ana mkataba na Malaga mpaka mwaka 2019 lakini imeripotiwa kuwa anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa dau dogo la kati ya kati ya Euro Milioni 10 na 12.

                                          
                                      

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kiungo wa Malaga kumrithi Cazorla Arsenal (+Video) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top