Manchester,England.
WAYNE Rooney amezima uvumi ulioenea kuwa anataka kuhamia China na badala yake amesisitiza kuwa nia na dhumuni lake kuu kwasasa ni kuendelea kubakia Manchester United.
Rooney,31,ametoka kauli hiyo muda mfupi baada ya wakala wake Paul Stretford kuripotiwa kuwa yuko nchini China akifanya mazungumzo na vilabu vya huko vilivyoonyesha nia ya kuitaka hudumu yake.
"Licha ya vilabu vingi kuonyesha nia ya kutaka kunisajili,jambo ambalo ni jema kabisa lakini napenda kutamka kuwa sina mpango wa kuondoka Manchester United kwasasa.
Mkataba wa Rooney klabuni Manchester United unaisha Juni 2018 na kumekuwa na uvumi kuwa hatapewa mkataba mpya pindi ule wa sasa utakapokwisha.
0 comments:
Post a Comment