Jedula,Hispania.
DAVID Collantes,mchezaji wa klabu ya ridhaa ya Jedula ya nchini Hispania, amekumbana na adhabu kali na ya aina yake baada ya kufungiwa kutocheza mechi 47 kwa kosa la kumchapa makonde mwamuzi msaidizi kwenye mechi yao ya wikendi iliyopita dhidi ya Portuense
Collantes anayecheza nafasi ya ushambuliaji alijikuta akitolewa uwanjani katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza kwa mchezo mbaya huku timu yake ikiwa tayari imeshalambwa mabao 3-0.
Wakati anatoka uwanjani ghafla Collantes alimvamia mwamuzi msaidizi ambapo alimtukana na kumchapa makonde matatu makali ,moja usoni na mawili mbavuni.
Wakati huohuo mshambuliaji huyo raia wa Hispania ameripotiwa kuwa alimkaba koo mwamuzi huyo pamoja na kumchana mdomo hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kumtia nguvuni Collantes.
Mbali ya kumfungia Collantes mechi 47 pia chama cha soka la ridhaa cha Hispania pia kimeripotiwa kuipoka pointi moja Jedula kwa kosa la kushindwa kumdhibiti mchezaji wao.
0 comments:
Post a Comment