728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 21, 2017

    Nahodha Wayne Rooney nje kikosi cha Man United kitakachoivaa Saint-Etienne Alhamis hii,yumo pia Ander Herrera.

    Manchester,England.

    LICHA ya kurejea mazoezini asubuhi ya leo huko Carrington,nahodha wa Manchester United,Wayne Rooney,ameachwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 kilichosafiri leo kuelekea nchini Ufaransa kuivaa Saint-Etienne kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya Europa ligi Alhamisi hii.

    Rooney,31,ameachwa nje ya kikosi hicho kutokana na kushindwa kupona kwa wakati maumivu ya misuli yaliyokuwa yakimkabiri katika siku za hivi karibuni.

    Wengine watakaokosekana kwenye kikosi hicho ni pamoja na Luke Shaw,Phil Jones na Matteo Darmian.

    Kiungo Ander Herrera pia ataukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

    Manchester United inaingia kwenye mchezo wa marudiano ikiwa kifua mbele baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wao uliochezwa Alhamis iliyopita huko Old Trafford. Mabao yote matatu ya Manchester United yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic.

    Kikosi kamili cha Man United kitakacho safiri kuifuata Saint-Etienne;

    De Gea, O'Hara, Romero;Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling,Valencia, Young, Carrick, Fellaini, Mata,Mkhitaryan, Pogba,Lingard,Schweinsteiger,Ibrahimovic, Martial, Rashford.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nahodha Wayne Rooney nje kikosi cha Man United kitakachoivaa Saint-Etienne Alhamis hii,yumo pia Ander Herrera. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top