728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 25, 2017

    Jamani nyie Robert Lewandowski ni zaidi ya Suarez,Costa na Karim Benzema.

    Munich,Ujerumani.

    BEKI wa zamani wa Bayern Munich,Lothar Matthaus,amesema staa wa klabu hiyo Robert Lewandowski ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani kwasasa hata zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez.

    Msimu huu Lewandowski amekuwa kwenye kiwango bora sana cha upachikaji mabao kwani mpaka sasa ameshapachika mabao 25 katika michezo 31.

    Matthaus anaamini kuwa kuna mengi zaidi kwenye soka la Lewandowski ukiachana na umahiri mkubwa wa kufunga mabao alionao nyota huyo wa kimataifa wa Poland.

    "Kwangu,Lewandowski ndiye namba tisa bora zaidi dunia," Ameandika Matthaus kwenye kalamu yake iliyochapishwa kwenye gazeti la Bild .

    Lewandowski ni bora kuliko wachezaji kama Karim Benzema na Luis Suarez.Straika wa Chelsea,Diego Costa pia anafunga mabao mengi na ni mmaliziaji mzuri.

    "Lakini Lewandowski amekuwa mchezaji mwenye mchango zaidi kikosini.Anafunga kwa mguu wake wa kulia, anafunga kwa mguu wake wa kushoto,anafunga kwa kichwa,anatoa pasi za mabao pia ni fundi wa kuchezea mpira.

    "Suarez ni mmaliziaji halisi lakini Lewandowski amezaliwa na uelewa fulani wa mchezo kitu ambacho kimekuwa kikimtofautisha na washambuliaji wengine.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Jamani nyie Robert Lewandowski ni zaidi ya Suarez,Costa na Karim Benzema. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top