London,England.
ARSENAL leo usiku itakuwa ugenini kucheza na Sutton United katika mchezo pekee wa hatua ya tano ya kombe la FA Emirates Cup lakini staa wake Danny Welbeck amejiondoa kikosini ili kukwepa uwezekano wa kuumia kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Gander Green Lane wenye nyasi bandia.
Welbeck ambaye jana Jumapili alikichezea kikosi cha Arsenal cha U-23 kwa dakika sabini pale kilipomenyana na Leceister City amesema ameamua kujiondoa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Sutton United kwa kuwa viwanja vyenye nyasi bandia kama ule Gander Green Lane huteleza sana na hivyo huwasababishia wachezaji majeraha.
Ikumbuke Welbeck amerejea dimbani hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomweka nje kwa takribani miezi minane.
Mshindi wa mchezo wa leo kati ya Arsenal na Sutton United atacheza na Lincoln City kwenye robo fainali itakayochezwa kati ya Machi 10 na 13.
0 comments:
Post a Comment