Kigali,Rwanda.
BAO la dakika ya 17 la mlinzi wa Zanaco,Taonga Bwembya limetosha kuitupa APR nje ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo mkali wa mkondo wa pili uliochezwa jioni ya leo huko Amahoro,Kigali.
Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa huko Lusaka,Zambia timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0.
Sasa hii ina maana kwamba Zanaco itacheza na mabingwa wa Tanzania,Yanga SC kwenye hatua inayofuata hapo Machi 11.Yanga SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2 dhidi ya Ngaya FC ya Comoro.Mshindi kati ya Yanga SC na Zanaco atatinga hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment