728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 20, 2017

    Simba,Yanga mmemsikia mkuu wa mkoa wa Iringa?

    Iringa,Tanzania.

    SIMBA na Yanga zimechimbwa mkwara bhana!!Mkuu wa mkoa wa Iringa,Amina Masenza, amezitaka Simba na Yanga kujiandaa na kichapo pindi zitakapokwenda mkoani hapo kucheza na Lipuli FC kwenye michezo yao ya ligi kuu bara msimu ujao.

    Masenza ameyasema hayo jana Jumapili wakati akiwapokea wachezaji wa Lipuli FC waliokuwa wakitokea jijini Mwanza walipokwenda kucheza na Pamba katika mchezo wa mwisho wa ligi daraja la kwanza.

    Masenza amesema Simba na Yanga zisitegemee kupata pointi za chee pindi zitakaposhuka kwenye dimba la Samora mkoani Iringa kucheza na Lipuli FC na badala yake zitarajie maumivu.

    Wakati huo huo Masenza amewataka wananchi wa Iringa kuwa na uzalendo na timu yao ya Lipuli FC na kuacha kuzishabikia timu za mikoa mingine kwani kufanya hivyo ni fedheha kubwa.Lipuli FC imerejea ligi kuu bara baada ya kupotea kwa miaka 16.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba,Yanga mmemsikia mkuu wa mkoa wa Iringa? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top