James Eduma.
Dar Es Salaam,Tanzania.
Wanachama na mashabiki wa Young Africans
wameombwa radhi kufuatia kupoteza mchezo wa wao wa siku ya jumamosi kwa
kukubali kufungwa na watani zao Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka
Tanzania bara.
Katibu mkuu wa Young Africans amewasilisha
kauli ya kuomba radhi kwa mashabiki na wanachama kwa niaba ya uongozi wa juu wa
klabu hiyo ambayo bado inaendelea kutetea ubingwa wa Tanzania bara.
Mkwasa amesema imeulazimu uongozi wa Young
Africans kufanya hivyo kutokana na kuamini kila mmoja alisikitishwa na matokeo
ya mchezo huo, ambao ulishuhudia wakiongoza bao moja kwa kipindi kirefu.
Hata hivyo mkwasa amesema kufungwa katika
mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba hakujawaondoa kwenye malengo ya kuendeleza
mazuri katika michezo mingine ya ligi kuu, hivyo amewataka wanachama na
mashabiki kuendelea kuwa wastahamilivu.
0 comments:
Post a Comment