Na Faridi Miraji.
Sergio Aguero amesema kwamba anataka kubaki Manchester City na amesisitiza kwamba ana mahusiano mazuri na kocha Pep Gaurdiola.
Muargentina huyo aliweka kambani mara mbili na kuisaidia City kutoka nyuma mara mbili na kushinda mechi ya UEFA dhidi ya Monaco kwa 5-3 jana usiku.
Aguero kwa muda mfupi alipoteza namba kwa Gabriel Jesus , na kuibua maswali kwamba ni jinsi gani ataingia kwenye mipango ya Guardiola na pia kama ataendelea kubaki Etihad.
Lakini Aguero ambaye ana mkataba mpaka mwaka 2020 amekanusha taarifa za yeye kutaka kuondoka City kwasababu ya kukalia benchi kwa kadhaa zilizopita.
"Mara zote nimekuwa nikisema kwamba nataka kubaki katika hii klabu, na mara zote nimekuwa nikisema kwamba mwishoni mwa msimu huu haitakuwa uamuzi wangu."
"Ukweli ni kwamba kuhusu vitu kama hivi,klabu ndio inashuhulikia kila kitu na ni lengo langu kubaki hapa."
Alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Guardiola, Aguero alisema," Ukweli ni kwamba tunapatana vizuri tu."
"Anachohitaji, juu ya kila kitu tena kutoka kwa wachezaji wote ni kuongeza juhudi zaidi. Mara zote huwa anahitaji mimi kujitoa zaidi, zaidi na zaidi."
0 comments:
Post a Comment