London,England.
Dimitri Payet ameanza kuisoma namba kama siyo kuionja joto ya jiwe
ikiwa ni siku chache tu tangu atangaze kuwa hataichezea tena Westham United baada ya klabu hiyo kumtilia ngumu kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Marseille.
Kwa mujibu wa gazeti la The Daily Mail la jana Ijumaa ni kwamba watu wanaodhaniwa kuwa ni mashabiki wa Westham United walivamia nyumbani kwa Payet,29,huko Essex jijini London na kwenda kuharibu gari la kifahari na nyota huyo wa Ufaransa kwa kuliponda na tofali lililovunja kioo na kuingia ndani.
Aidha habari nyingine zinasema kuwa Payet ametengwa na sasa anafanya mazoezi na kikosi cha vijana cha Westham United huku kukiwa na habari pia kuwa ameondolewa kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa Westham United ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupashana habari mbalimbali ikiwemo kupanga ratiba za mitoko ya mlo wa jioni
Wakati huohuo Westham United imeripotiwa kuwa na mpango na kuishitaki Marseille,FIFA,kwa madai kuwa inatumia mbinu chafu kujaribu kumsajili Payet.
0 comments:
Post a Comment