728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 23, 2016

    Simba wagoma kucheza na Yanga, Wataka Marefa wa Nje ya Nchi

    Viongozi wa klabu ya simba umesema hautacheza mchezo wowote wa ligi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga endapo waamuzi hawatatoka nje ya nchi tena wenye uzoefu wa mechi kubwa wanaotambuliwa na Fifa.
    Simba wapo tayari kulipa gharama za waamuzi hao kuanzia mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili ili haki itendeke kwakua watani wao wamekuwa wakipendelewa mara kwa mara na marefarii wa hapa nchini.
    Msimamo huo umetolewa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari klabuni hapo na kusema kuwa kwasasa hawatakuwa tayari kuona haki zao zikidhulumiwa kwa namna yoyote na wataanzia mzunguko wa pili unaotarajia kuanza Disemba 17.
    "Kila mtu aliona jinsi mwamuzi Jonensia Rukyaa alivyotunyonya msimu uliopita na Matrin Saanya mechi iliyopita sasa hatutaki muamuzi yoyote wa Tanzania kwenye mechi dhidi ya Yanga. Mechi ya Zamalek na Al Ahly waamuzi wanatoka nje ya Misri na sisi tunataka hivyo " alisema Manara.
    Wakati huo Manara ameishangaa kamati ya masaa 72 ya shirikisho la mpila wa miguu nchini TFF kuendelea kufanya Uchunguzi juu ya sakata la Samuel Mpenzu wakati mengine tayari wametoa maamuzi na adhabu pia.
    " Tangu mchezo watu na Yanga hadi leo ni siku 53 zimepita lakini bado Uchunguzi unaendelea, makocha wa Azam na Yanga timu pamoja na wachezaji waliofanya makosa mzunguko wa kwanza wamepata Adhabu kwanini suala la Saanya hadi leo linasubiri Uchunguzi ? "alihoji Manara.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba wagoma kucheza na Yanga, Wataka Marefa wa Nje ya Nchi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top