Nairobi,Kenya.
ALIYEKUWA kocha mkuu wa zamani wa klabu ya Azam FC,Mwingereza Stewart Hall,jana Jumatatu alitambulishwa rasmi kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya AFC Leopards ya Kenya.
Hall aliyeachana na Azam FC mwezi Agosti mwaka huu amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa AFC Leopards inayoshikilia nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Kenya.Pointi 8 juu ya mstari wa kushuka daraja.
AFC Leopards imeamua kumwajiri Hall baada ya hivi karibuni kumtupia virago aliyekuwa kocha wake mkuu Mbelgiji Ivan Minnaert kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwenye michezo ya ligi kuu ya nchi hiyo.
Mwenyekiti wa AFC Leopards,Dan Mule,amesema klabu yake imeamua kumwajiri Hall kutokana na ukweli kwamba kocha huyo wa zamani wa klabu ya Sofapaka ana ufahamu mkubwa na mchezo wa soka na anaamini atairejesha AFC Leopards kwenye makali yake ya zamani.
0 comments:
Post a Comment