728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 13, 2015

    SAFIII!!YANGA YAMKABIDHI GARI SAFI MALIMI BUSUNGU

    Mshambuliaji mpya wa Yanga,Malimi Busungu,sasa anatamba katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam akiwa na gari lake Toyota IST alilokabidhiwa muda mfupi tu baada kujiunga na timu hiyo.

    Busungu alijiunga na Yanga hivi karibuni kwa dau la usajili la Sh milioni 25 akitokea Mgambo JKT ya Tanga ambayo aliichezea kwa mafanikio msimu uliopita.

    Busungu amesema anatumia gari hilo katika mizunguko yake ya kawaida ndani ya Dar es Salaam na anajisikia furaha kuwa nalo.

    “Nashukuru Mungu gari langu nimeshapewa na sasa napiga nalo misele na ukinikuta kwenye daladala basi nimependa mwenyewe au kuna tatizo, kazi iliyobaki ni kuthibitisha thamani yangu kwa Yanga,”alisema Busungu.

    Straika huyo kwa sasa yupo katika kambi ya kikosi cha mjumuisho cha Taifa Stars ambacho kimebaki jijini
    Dar es Salaam kikifanya mazoezi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAFIII!!YANGA YAMKABIDHI GARI SAFI MALIMI BUSUNGU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top