Habari na Paul Manjale
Michuano ya kombe la mataifa bingwa barani Amerika ya kusini maarufu kama "Copa America"yaliendelea tena usiku wa kuamkia leo jumapili juni 14 kwa miamba ya kundi B kushuka dimbani kupepetana.
Katika mchezo uliopigwa katika dimba la Estadio Portada huko La Selena Argentina ikiwa na wakali wake wote ilijikuta ikishindwa kuhimili vishindo toka kwa vijana wa Paraguay na kutoka sare ya bao 2-2.
Argentina ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Sergio Aguero na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati.
Kipindi cha pili vijana wa Paraguay walikuja na kasi mpya ambayo iliwafanya Waargentina washindwe kuendana nao na hatimaye wakaruhusu mabao 2 kupitia kwa Nelson Haedo Valdez na Lucas Barrios.
Katika mchezo mwingine wa kundi B,mabingwa mara 13 wa michuano hiyo Uruguay walianza vyema kuutetea ubingwa wao walioutwaa 2011 baada ya kuinyuka Jamaica kwa goli 1-0 kupitia kwa mshambuliaji Cristian Rodriguez.
Baada ya matokeo hayo Uruguay inaongoza kundi ikiwa na alama 3 huku Argentina na Paraguay zikifuatia kwa pamoja zikiwa na alama 1,Jamaica inaburuza mkia.
Leo jumapili ni zamu ya kundi C
Colombia v Venezuela
0 comments:
Post a Comment