728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 14, 2016

    MEDEAMA FC YAICHAPA TP MAZEMBE NA KUKARIBIA NUSU FAINALI SHIRIKISHO


    Sekondi,Ghana.

    MEDEAMA FC imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni hii kuichapa TP Mazembe kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo mkali wa kundi A wa hatua ya nane bora uliochezwa katika uwanja wa Episong Sports-Medeama,Ghana.

    MedeamaFC ilianza kuonyesha dhamira ya kuibuka na pointi zote tatu za mchezo huo baada ya Enoch Atta Agyei kufunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa faulo.

    Medeama FC ikicheza kwa kujiamini na kushambulia ilifanikiwa kupata mabao mengine kupitia kwa Kwasi Donsu na Moses Sarpong.

    Mabao ya TP Mazembe yamefungwa na Jonathan Mpangi pamoja na Rainford Kalaba.

    Matokeo hayo yameifanya Medeama FC ichupe mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha alama nane.TP Mazembe inaongoza ikiwa na alama 10.Mo Bejaia iko nafasi ya tatu na alama zake tano.Yanga iko mkiani na alama zake nne.Timu zote zimecheza michezo mitano kila mmoja.

    Medeama FC inahitaji ushindi au sare katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ili iweze kutinga nusu fainali.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MEDEAMA FC YAICHAPA TP MAZEMBE NA KUKARIBIA NUSU FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top