Pretoria,Afrika Kusini.
Mamelodi Sundowns imeendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu ya afrika Kusini maarufu kama Absa Premiership baada ya Jumamosi usiku kuichapa Kaizer Chiefs kwa mabao 3-1 nyumbani Loftus Versfeld,Pretoria.
Wageni Kaizer Chiefs ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya mlinzi Lorenzo Gordinho kufunga kwa kichwa dakika ya 30 akiuganisha kona ya George Maluleka.Kuingia kwa bao hilo kuliwaamisha wenyeji Mamelodi Sundowns ambao walikuja juu na kufanikiwa kupitia kwa Leonardo Castro,Thabo Nthethe na bao la kujifunga la Willard Katsande.
Sundowns sasa wamefikisha pointi 62 wakiwa kileleni baada ya Kucheza michezo 27 wakati Chiefs wao wamebaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 44.
Vikosi
Mamelodi Sundowns: 36 Onyango, 6 Arendse, 4 Langerman, 2 Nthethe, 16 Mphahlele, 33 Mabunda, 7 Dolly (Malajila 82'), 19 Mashaba (Modise 90'), 25 Castro,20 Billiat (Zwane 71'), 8 Kekana
Kaizer Chiefs: 32 Khune, 18 Moleko, 26 Gordinho, 3 Mathoho, 23 Ritchie, 31Katsande, 12 Maluleka (Twala 57'), 6 Letsholonyane, 17 Lebese (Manqele 71'), 25 Parker, 14 Tshabalala
0 comments:
Post a Comment