Barcelona,Hispania.
Bao la dakika ya 81 alilofunga Luis Suarez Jumamosi usiku na kuisaidia Barcelona kuichapa Real Betis mabao 2-0 huko Benito Villamarin limemfanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool kufikisha mabao 35 na kuwa mmoja kati ya wachezaji sita waliowahi kufunga mabao 35 na zaidi katika msimu mmoja wa ligi ya La Liga.
Bao hilo pia limemfanya Luis Suarez awe mchezaji wa pili wa Barcelona baada ya Lionel Messi kufikisha idadi hiyo ya mabao katika msimu mmoja.
Wengine waliowahi kufikisha idadi hiyo ya mabao ni Lionel Messi mara tatu,Cristiano Ronaldo mara tatu,Hugo Sanchez 1988-89,Baltazar 1988-89 na Telmo Zarra 1950-51.
0 comments:
Post a Comment