Liverpool,England.
KAMWE SIWEZI!!Kocha mkuu wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp anaamini hata iweje hawezi kupewa kazi ya kuinoa Bayern Munich kwa sababu aliicheka miamba hiyo ya Allianz Arena ilipochapwa na Mainz hapo mwezi Machi mwaka huu.
Akifanya mazungumzo na kituo cha 11Freunde Klopp amedai kicheko alichokiangua baada ya Bayern kuchapwa mabao 2-1 na Klabu yake ya zamani ya Mainz mwezi Machi kimefunga milango ya yeye kuja kuwa kocha wa miamba hiyo siku moja.
"Ni kosa langu,nimeufunga mwenyewe mlango wa kuja kuinoa Bayern.Ilikuwa ni furaha kutokana na mafanikio ya Mainz,picha za video zimeonyesha nilikuwa na furaha kupindukia.Nimeharibu."
Klopp aliichezea Mainz katika kipindi chake chote cha uchezaji kabla ya kupewa kibarua cha kuino mara tu baada ya kustaafu.
0 comments:
Post a Comment